Madai ya Mh.Lema kugoma kula hayana mashiko

Mh mbunge wa Arusha mjini amegoma kula tangu amewekaa maabus zinaendelea kusambaa kwa kasi,hiii ni baada ya maelezo yaliyotolewa na meya wa jiji la arusha bwana Calist Lazaro ambapo amesema Mh.Lema amelazimika kugoma kula baada yakutoridhika na ukamatwaji wake ambao ameutafsiri kama udhalilishwaji mbele ya familia yake.

Nalazimika kusema madai ya muheshimiwa mbunge Kugoma kula niyamsingi ila ameyafanya kwa kukurupuka,kiasi chakukosa mashiko,haswa kwa wanaomshikilia, mh lema Hajatuambia ni nini hasa anataka afanyiwe ili arejee kula kama kawaida,alipaswa kuliambia Jeshi la Polisi kama walimkamata kwakumdhalilisha mbele ya familia yake,basi polisi Wakaombe radhi kwa familia na watoto wake ndio arejeshe hali yake ya kula kama kawaida,

Niwazi watu wote wanaotumia njia hii kudai haki huweka masharti ambayo yakitekelezwa hurejea kula kama kawaida,mh Mbunge hoja yake ya msingi lakini ameishia kusema amegoma kula Kwa sababu amekamatwa kwakudhalilishwa mbele ya familia yake,ingependeza kama angeenda mbali zaidi kuliambia Jeshi la Polisi lifanye jambo gani ili arejee kula kama kawaida.

Baada ya kusema hayo naomba nimpe pole za dhati mh lema,sote tunafahamu maabusu sio pazuri Mh LISU alikaaa siku moja akatupa ushuhuda MAABUSU sio pazuri,LEMA umekaa siku Tatu tunakila sababu kukupa Pole.

Nawasilisha

MKAPA Apongezwa Kuwakutanisha Rais Magufuli na Lowassa

BAADHI ya viongozi wa dini na wasomi, wamempongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwa hatua yake ya kuwakutanisha Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Wamesisitiza kuwa hatua hiyo, inaonesha jinsi ambavyo demokrasia na amani imekomaa nchini. Viongozi hao walikutana juzi katika Misa Takatifu ya kuadhimisha Jubilee ya Miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Mkapa na mkewe, Anna, iliyofanyika juzi kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay, Dar es Salaam.

Viongozi wa dini waliozungumza na gazeti hili na kupongeza hatua hiyo ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba la Kanisa Katoliki, Mhashamu Methodius Kilaini, Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry, Dk Charles Gadi na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum.

Kwa upande wa wasomi, gazeti hili lilizungumza na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana na Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Mwingine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu.

Maoni ya viongozi wa dini Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Askofu Kilaini alisema jambo walilolifanya viongozi hao ni la kuungwa mkono na Watanzania wote.

“Jambo hili tumeliona na tumelifurahia sana na inatupa funzo kwamba tunapofanya siasa, tusisahau utu wetu. Siasa tuiache kama siasa… pia tumejifunza kwamba siasa si uhasama kwa sababu viongozi hawa wameweza kukutana na kupeana mikono,” alisema.

Alisema; “Mtu unapopeana mkono na mtu na kuangaliana usoni inaonesha kwamba hakuna uadui kati yenu hivyo kwa viongozi hao wameonesha kwamba wanakinzana katika siasa tu...” alisema.

Askofu Kilaini alisema, wanaamini kwamba kukutana kwa viongozi hao ambao wana mrengo tofauti ni mwanzo mzuri wa maridhiano ya pande zote mbili ambazo zimekuwa na misuguano ya kisiasa.

“Nawashauri Watanzania wenzangu kwamba kama viongozi wetu wakuu wameweza kukutana na kupeana mikono na kusalimiana tena na kupiga picha ya pamoja wakiwa karibu basi na sisi wafuasi wao tusijengeane chuki bali tupendane… tusiendelee kusigana na kupigana maana viongozi wetu wenyewe wanaelewana ila wanatofautiana tu katika siasa,” alisema.

Kwa upande wake, Askofu Gadi alisema kwa viongozi hao kukutana wanaamini kwamba maombi wanayoyafanya yanazidi kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa nchi.

“Watanzania tuzidishe maombi maana yana nguvu na kupitia maombi hata yasiyowezekana yanawezekana, viongozi wa dini tuombe sana na tuhamasishe watu waombe maana hata hawa viongozi wetu ni waumini wetu na ni washiriki wazuri wa nyumba za ibada na tunashika nafsi zao,” alisema.

Aidha alisema viongozi hao wameonesha kwamba ni watu wanaomuogopa na kumheshimu Mungu kwa kusalimiana kwa upendo na kusisitiza kwamba maombi huleta upatanisho na kubadilisha jamii.

Alisema kupitia kanisa hilo, wamekuwa wakifanya huduma ya maombi mara kwa mara ambapo kwa sasa wameanza maombi ya siku 1,001 na wiki iliyopita walifanya maombi wilayani Chato mkoa wa Geita kwa ajili ya kumuombea Rais Magufuli katika utendaji wake.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa alisema tukio hilo ni la heri, kwa kuwa watu walikuwa wakiwatazama viongozi hao kama maadui, hivyo kwa kupeana mikono wameithibitishia jamii kwamba wanatofautiana tu katika siasa.

“Walichokifanya viongozi wetu wameonesha kwamba, siasa si uadui na tunaomba kukutana huko kuwe heri na waendelee kukutana mara kwa mara kwa ustawi wa Taifa letu,” alisema.

Wasomi nao wafunguka Katika hatua nyingine, wasomi nao walieleza kupongeza kitendo hicho kilichowakutanisha walikuwa wapinzani wa karibu wakati wakigombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Rais Magufuli na Lowassa.

Kwa namna ya pekee wasomi hao walipongeza pia kitendo hicho cha kizalendo, ambacho viongozi hao walikionesha kwa kushikana mikono, kutabasamu na kuonekana wakiteta kwa nyuso za tabasamu.

Profesa Baregu mbali na kupongeza uzalendo huo, alisema kukutana na kuzungumza kwa Rais Magufuli na Lowassa ichukuliwe kuwa ni fursa kwa viongozi hao, ambayo wanapaswa kuitumia kufanya mazungumzo ya kuimarisha amani.

“Hiyo itafsiriwe kuwa ni fursa ambazo huwa inajitokeza katika mazingira tofauti, aidha kwa kupangwa au bila kupangwa, lakini kikubwa watumie fursa hiyo vilivyo,” alisema Profesa Baregu. Alisema kukutana kwa Rais Magufuli na Lowassa ni fursa nzuri kwani walikuwa hawajawahi kukutana tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba, mwaka jana.

Alisema mambo machache ambayo viongozi hao walizungumza juzi katika muda mfupi, yataweza kutumika vizuri kutatua mambo ya kisiasa ambayo yanaendelea hapa nchini kwa sasa na kufungua njia nzuri.

“Na hii inaweza kuwa njia nzuri kuzungumzia masuala ya kisiasa, demokrasia na pia Katiba mpya ambayo ndio kilio kikubwa cha Watanzania ili tuweze kupata Katiba mpya,” alisema Profesa Baregu.

Msomi huyo alisema pia fursa hiyo itumike kuleta amani kwa wananchi na kwa maana ya kupatikana maridhiano katika masuala ya kisiasa.

Profesa Mkumbo alimpongeza Mkapa kwa kitendo hicho cha kuwakutanisha viongozi hao na pia kuwapongeza Rais Magufuli na Lowassa kwamba pamoja na walikuwa katika mchuano mkali katika Uchaguzi Mkuu uliopita na mwisho Rais Magufuli kupata ushindi, lakini wameonesha bashasha ya aina yake.

“Huo ndio utanzania ambao Watanzania wanautaka, tunaweza kutofautiana bila kugombana, utanzania wetu haujali dini, kabila wala kitu kingine chochote,” alisema Profesa Mkumbo.

Aidha alisema muonekano pia wa viongozi hao wawili, ulionesha wazi walikuwa katika hali ya amani, “hata muonekano wao uliweza kuona kabisa ilikuwa safi, na Rais wetu kama tunavyomjua si mtu wa kuficha jambo lakini walicheka na kuzungumza vizuri.”

Kwa upande wake, Dk Bana alisema kwa muonekano ambao walionesha viongozi hao wawili jana ilionesha changamoto za kisiasa zilizokuwepo, hazitaendelea kuwepo tena kwani viongozi hao walionekana kuteta kwa upendo.

“Ile inaonesha kabisa harakati za Ukuta (Umoja wa Kupambana na ‘Udikteta’ Tanzania) hazipo tena na jana (akimaanisha juzi) zilizikwa pale, walionekana kunong’ona na kupeana mikono kwa amani kabisa na inaonesha wote ni wamoja katika kujenga nchi yenye amani,” alisema Dk Bana.

Alisema nasaha ambazo zilitolewa pia viongozi wa dini katika hafla ile, zitumike pia vizuri katika kuondoa masuala yote ya kisiasa, ambayo yamekuwa yakileta mvutano na badala yake kujenga upendo na amani. Alisema uwazi wa Rais Magufuli na maneno aliyozungumza, yalikuwa ya busara.

Lema Aendelea Kugoma kula akiwa mahabusu, Mwanasheria Wake Kufungua Kesi Mahakama Kuu Leo

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Lema alikamatwa siku hiyo saa 12 alfajiri akiwa nyumbani kwake, Njiro,  na hadi sasa anashikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.

Kutokana na kuendelea kugoma kula, Wakili wake, John Mallya amesema leo saa sita mchana atakwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufungua kesi ya kutaka mteja wake afikishwe mahakamani.

Malya jana alisema katika kesi hiyo atashirikiana na Chadema kuwashtaki mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mkoa wa Arusha.

Tangu mbunge huyo akamatwe amegoma kula kwa  kile anachodai kupinga udhalilishwaji aliofanyiwa na polisi wakati wa kukamatwa.

Pia, Lema anasema alinyanyaswa mbele ya watoto wake nyumbani kwake huku wakijua yeye ni kiongozi na amechaguliwa na wananchi.

Neema, mkewe Lema,jana alithibitisha kwamba  mumewe amegoma kula.

“Anaendelea kugoma kula mpaka sasa kwa sababu  hata sasa nimetoka polisi asubuhi kumpelekea chakula, lakini amekataa kula.

“Lakini nilipouliza pale polisi kuwa wanampeleka lini mahakamani, nilijibiwa wanaendelea kumhoji,”alisema Neema.

Juzi, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alithibitisha kukamatwa kwa Lema na kueleza kuwa alihojiwa dhidi ya matamshi ya uchochezi na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika   uchunguzi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkumbo, Lema anatuhumiwa kuwachochea wakazi wa Arusha kuandamana Septemba mosi, mwaka huu kuhamasisha kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).
Older Posts
© Copyright VIDEO
Back To Top