the municipal direct crying after huge question from LAAC

KUPATA PICHA ZA KUCHEKESHA WHATSAPP BOFYA HAPA CHINI

Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos below Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos below

Kibano chamtoa chozi mteule wa Magufuli


MKURUGENZI Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya jana aliangua kilio alipokuwa akihojiwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) hapa Dodoma.




MKURUGENZI Mtendaji mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Agnes Mkandya.
Julai 7, mwaka huu, Rais John Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji matano, manispaa 21, miji 22 na wilaya 137 za Tanzania Bara.

Kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 walitoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wapya.

Mkandya alilia baada ya kupata wakati mgumu, kutokana na kubebeshwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha ndani ya wilaya hiyo kama ilivyoainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14.

Mkandya alijikuta akibubujikwa machozi alipokuwa akihojiwa na kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake na Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), Vedasto Ngombale.

Mkurugenzi huyo alifikwa na hali hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Leah Komanya, aliyetaka kujua pamoja na halmashauri hiyo kuwa na sera ya kukabiliana na vitendo vya ubadhirifu wa fedha, imejipangaje kwa kuwa wana ubadhirifu upande wa uhasibu.

Komanya pia alimtaka Mkurugenzi aeleze ni kwa nini halmashauri imekuwa ikishindwa kujipanga katika kusimamia mapato na ina mpango gani wa kuunganisha mfumo wa udhibiti wa ndani.

“Ubadhirifu huu (ndani ya halmashauri) unatokana na halmashauri kutofunga mfumo wa kielektroniki,” alisema Komanya.
Mkurugenzi huyo alisema yeye ni mgeni katika halmashauri hiyo, na kwamba aliikuta ikiwa na uchafu mkubwa kutokana na kuwapo kwa watumishi wabadhirifu.

Sambamba na hilo, wajumbe wa LAAC walitaka kujua sababu za fedha kwa ajili ya wanawake na vijana kutokwenda kwa walengwa wakati zilikuwa zimetengwa Sh. milioni 30 kwa mwaka huo, lakini zilizopelekwa ni Sh. milioni tatu tu.

Akijibu hoja hizo, Mkurugenzi huyo alijikuta akishindwa kumalizia kujibu na kuangua kilio huku akisema mashine 20 za mfumo wa kielektroniki tayari zimenunuliwa na wanasubiri Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL) kufunga mfumo huo.

Aidha, Mkandya alisema wakuu tisa wa idara katika halmashauri hiyo wamesimamishwa kazi kutokana na ubadhirifu, kabla ya kushindwa kumaliza kutoa maelezo na kuanza kulia akidai halmashauri hiyo ina matatizo makubwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilianzishwa baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa katika serikali ya Rais wa nne, Jakaya Kikwete.

BOFYA HAPA CHINI KUONA VITUKO VYA MASTAA BONGO MOVIES

;

WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

Newer Posts Older Posts
© Copyright VIDEO
Back To Top