KUPATA PICHA ZA KUCHEKESHA WHATSAPP BOFYA HAPA CHINI
Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos below Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos belowGeuza Smartphone Yako Kuwa Computer
Unajua Kama Ukiwa Na Smartphone Unaweza Kuigeuza Ikawa Computer?
Leo Nimekuja na kitu kizuri!
Ni moja ya mambo ya Ukuaji wa teknolojia, hivyo basi sio mbaya baada ya kukushirikisha ukamshirikisha na mwenzako pia;
- Ulishawahi kuhisi kuichoka simu au tablet yako kutokana na udogo wake kwenye kuhifadhi mambo yako? (low storage space)
- Muda mwingine inakusumbua na kukwambia memory is full huwezi kuweka kitu chochote
- Simu yako imejaa vitu vyako vya muhimu sana na hauna Computer na hautaki kuvifuta na pengine hauna sehemu ya kuvitunza
- Ukisoma
maelezo vizuri utagundua vingi na utapata njia ya kutatua matatizo
mengine mengi pengine hata yakazidi hayo niliyoyataja hapo
Ok, sasa basi ninakupa hii kitu hapa, Kuna Cable Mpya kabisa zimetoka juzi juzi zinaitwa “OTG Cables“, kirefu cha OTG ni (On The Go) Kwa hiyo kwa kirefu zinaitwa On The Go Cables, Hizi
Cable kuna watu hawazifahamu kabisa na hawajui utamu wake. Leo
nakudadavulia mambo makubwa utakayoweza kuyafanya endapo una OTG Cable, itazame hapa;


Cable hizi zina pande mbili,
Upande wa
kwanza una kichomekeo kama Cha zile chaji za smartphones zetu
tulizozizoea, na huu ndio upande unaoingia kwenye simu au tablet na
unachomeka kama vile unavyochomeka chaji.
Na upande wa pili wa OTG Cable kuna tundu kubwa la kuchomekea vitu vya asili za USB kama vile flash, lakini kwa upana zaidi naomba nieleze maana kuu ya hili tundu (kwa kitaalamu huwa tunaliita USB Female Port), na linaruhusu kuchomekwa vifaa mbalimbali kwa matumizi tofauti tofauti ila tu vifaa hivyo viwe vya aina ya USB, mfano kama Flashi, Keyboard, External Hard Disk, Speakers n.k.
Sasa basi
ukichomeka Cable hiyo kwenye simu au tablet yako kama vile unavyochomeka
chaji kwa upande wa kwanza na upande ule wa pili ukachomeka flash, basi
utaweza kuisoma kwa ndani ya simu kama vile huwa unasoma memory card
yako, tazama picha hapa chini kuelewa zaidi;
Unaweza
pia kuchomeka External Hard Disk na ukaitumia kwenye simu au tablet
yako, kufanya shughuli mbalimbali kama vile kucheki movies n.k, sijamaliza bado;
Unaweza
pia kuchomeka External Hard Disk na ukaitumia kwenye simu au tablet
yako, kufanya shughuli mbalimbali kama vile kucheki movies n.k, sijamaliza bado;
Kama simu au tablet yako imejaa vitu unaweza kuvihamishia kwenye flash ukavitunza, kwa mfano hauna Computer, unaweza kununua OTG Cable na flash yako ya 16 GB ukaweka vitu vyako kama Picha, Videos
n.k na simu yako ikabaki free na ikawa na spidi ile ile kama ya siku
ile ulipoinunua, na hapa hautalalamika tena kuwa simu yako ina uwezo
mdogo wa kutunza vitu, sijamaliza bado;
Kwa wale tunaotamani sana kuwa na Computer lakini hatuna uwezo
wa kuzinunua, lakini tunamiliki Smart Phones Zetu nzuri tu, basi hapa
nakupa maujanja, nenda dukani ulizia OTG Cable (Sijui ni duka gani maana
simtangazii mtu biashara ila mimi binafsi nilinunua elfu 5 tu ila kuna
sehemu ukienda utapigwa mpaka elfu 40, tembelea duka lolote la simu
ulizia), ukishanunua OTG Cable,
nunua flash zako za 16 GB kama 3 au 5 kama una uwezo, kisha nenda
kakopi vitu unavyohitaji kwa mtu mwenye Computer na uviweke kwenye flash
yako (mfano flash ya Movies pekeyake, ya madocuments pekeyake, ya
miziki pekeyake na ya picha pekeyake, najua ugonjwa wetu vijana na wazee
kwa mbaliii ni Miziki, Movies, Kujirekodi Na kupiga Picha hasa kwenye
event za kifamilia na hivi vitu hujaza sana simu zetu, hivyo ukiwa na
flash zako kama nivyoeleza basi utakuwa salama zaidi, ukiweza hayo basi
Ukiwa na simu yako, flash zako, na hiyo OTG Cable ni sawa na kumiliki Laptop, sijamaliza bado;
Utaepuka
maswala ya kuhamisha vitu kwa kuchomeka USB cable, au kutumia bluetooth
kuhamishiana vitu vyenye saizi kubwa na vingi toka kwenye simu au tablet
ya mtu mwingine bali litakuwa ni swala zima la kuchomeka OTG Cable na flash yako kisha unahamisha vitu kwa kukopy na kupaste, na zina spidi nzuri balaa, sijamaliza bado;
Wale wenye simu kubwa unaweza kuikamilisha simu yako kuwa Computer kwa kuifanya hiyo OTG Cable iweze kuzalisha USB ports nyingine nyingi ili uweze kuchomeka vifaa vingi kwa wakati mmoja kama Speaker, keyboard, mouse, external hdd n.k, angalia picha hapa chini;


Jamani kuna mengi
yanakuja mazuri tu usisahau kuwa unatembelea na site hii kwani kuna
mengine yatakupita, kwa wale wa mikoani mnaohitaji kujifunza Ufundi wa
Computer kwa njia ya Mtandao soma kila kitu kisha nitafute tuyajenge,
nakutakia Jumapili njema.
BOFYA HAPA CHINI KUONA VITUKO VYA MASTAA BONGO MOVIES
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

