SIMBA YAANZA MSIMU MPYA WA VPL KWA POINTI 3

KUPATA PICHA ZA KUCHEKESHA WHATSAPP BOFYA HAPA CHINI

Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos below Always visit the site for enjoying the funny and all comedy releted videos, because my purpose is to see yoou happy all the time, after watching i beg you to share my videos with friends, be happy all the time and enyoy the videos below
Mfungaji wa bao la pili la Simba Fredrick Blagnon akipongezana na Laudit Mavugo
Mfungaji wa bao la pili la Simba Fredrick Blagnon akipongezana na Laudit Mavugo
Simba imeuanza vyema msimu wa ligi kuu Tanzania bara kwa kupata ushindi wa magoli 3-1 mbele ya Ndanda FC ya Mtwara katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2016/17 mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa.
Mshambuliazi mpya wa Simba Laudit Mavugo alianza kuifungia klabu yake bao la kuongoza dakika ya 19 kipindi cha kwanza kabla ya bao hilo kusawazishwa na Omary Mponda dakika ya 36.
Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana bao 1-1.
Winga wa Simba Jamal Mnyate (kushoto) akiwania mpira na kiungo wa Ndanda FC Kiggi Makasi
Winga wa Simba Jamal Mnyate (kushoto) akiwania mpira na kiungo wa Ndanda FC Kiggi Makasi
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (katikati) akipambana kuwatoka mabeki wa Ndanda FC
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (katikati) akipambana kuwatoka mabeki wa Ndanda FC
Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji kwa kuwapumzisha wachezaji kadhaa na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji wengine.
Ndanda ilimpumzisha Aziz Sibo ambaye aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na Bakari Mtama wakati Nassoro Kapama aliingia kuchukua nafasi ya Shija Nkiwa.
Golikipa wa Ndanda FC Jackson Chove akipatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu hiyo baada ya kuumia wakati wa mchezo wa VPL dhidi ya Simba
Golikipa wa Ndanda FC Jackson Chove akipatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu hiyo baada ya kuumia wakati wa mchezo wa VPL dhidi ya Simba
Simba wao waliwatoa Ibrahim Ajib ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Fredrick Blagnon, Mwinyi Kazimoto aliingia kuchukua nafasi ya Jamal Mnyate.
Fredrick Blagnon akaifungia Simba bao la pili dakika ya 74 kabla ya Shiza Kichuya kukamilisha ushindi kwa kukwamisha kambani bao la tatu.
Beki wa Ndanda FC (hini) akimiliki mpira mbele ya Shiza Kichuya
Beki wa Ndanda FC (hini) akimiliki mpira mbele ya Shiza Kichuya
Jamal Mnyate akiachia shuti katikati ya mabeki wa Ndanda FC
Jamal Mnyate akiachia shuti katikati ya mabeki wa Ndanda FC
Dondoo muhimu
  • Mavugo na Blagnon wamefunga magoli yao ya kwanza kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.
  • Goli la Mavugo ni la pili katika mechi tatu alizocheza akiwa Simba. Bao lake la kwanza lilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, mechi ya pili ilikuwa dhidi ya URA ya Uganda ikiwa ni mechi ya pili ya kirafiki ya kimataifa.
  • Salum Telela amecheza mechi yake ya kwanza kama kwenye ligi akiwa nje ya Yanga tangu alipoachana na mabingwa hao watetezi wa VPL baada ya mkataba wake kumalizika.

BOFYA HAPA CHINI KUONA VITUKO VYA MASTAA BONGO MOVIES

;

WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

Newer Posts Older Posts
© Copyright VIDEO
Back To Top